KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte na nyota wake Marco Alonso na Danny Drinkwater watawania tuzo za kung’ara Ligi kuu England Desemba, mwaka jana. Conte ametajwa miongoni mwa watakaogombea tuzo ya kocha bora wa mwezi. Chelsea ilifanya vizuri mwezi Desemba kwani ilishinda mechi tano, ilitoka sare moja na kupoteza mchezo mmoja. Drinkwater atawania tuzo ya goli bora la mwezi kutokana bao maridadi alilofunga kwenye mechi dhidi ya Stoke City, mwezi Desemba. Alonso naye alikuwa moto wa kuotea mbali kwani aliisaidia timu hiyo kutoruhusu bao mechi nne na alifunga mabao mawili kwenye mechi za dhidi ya Brighton na Southampton. Washindi wa tuzo hizo hupatikanakupitia uchambuzi wawataalamu wa soka, kura za mashabiki na manahodha wa timu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here