KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amekuna kichwa na amepata dawa ya matatizo ya timu hiyo, ambayo katika siku za karibuni ilionekana kama imepoteza mwelekeo. Mourinho aliiongoza Manchester United kuifunga Everton 2-0 ugenini na kumaliza mwenendo mbaya timu hiyo kwenye Ligi Kuu England katika siku za karibuni. Manchester United kabla ya mchezo wake na Everton, siku ya mwaka mpya ilikuwa imetoa sare tatu mfululizo na Leicester City, Burnley na Southamptom. Pia ilitolewa kwenye robo fainali ya Kombe la Carabao na Bristol City. Na kibaya zaidi Manchester United yenye pointi 45 kwenye nafasi za juu imejikuta kwa sasa inakabana koo na Chelsea kuwania nafasi ya pili kwani Manchester City inapepea katika uongozi wa ligi ikiwa na pointi 62. Mourinho abadili fomesheni Moja ya mambo ya Mourinho anayolaumiwa ni kushindwa kumtumia kiungo wake wa bei mbaya, Paul Pogba. Mourinho tangu amnunue Pogba kwa bei ya rekodi ya dunia ya pauni milioni 89, alipenda kumchezesha kama kiungo lakini akifanya majukumu ya ulinzi zaidi. Mara chache ndio amekuwa akimpatia nafasi ya kuwa huru na kuchezesha timu. Hali hiyo ilifanya watu wengi wamwone kama Pogba alikuwa wa kawaida tu lakini sio wa kununulia kwa fedha nyingi. Pamoja na ukweli kuwa Pogba hufanya kazi nzuri zaidi katika kupandisha mashambulizi ya Manchester United lakini bado Mourinho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here