Kocha mpya wa Simba Raia wa Ufaransa, Pierre Lichantre.

KOCHA mpya wa Simba, Pierre Lachantre leo atakuwa Uwanja wa Taifa kuishuhudia Yanga ambayo anachezea mshambuliaji Ibrahim Ajibu ikiumana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu.

Kocha huyo ataongozana na msaidizi wake, Aimen Mohammed Habib lakini Yanga wameonya juu ya ujio wa kocha mkuu.

Kitakwimu Pierre anaonekana yuko vizuri lakini baadhi ya wachezaji wa Yanga wamewatahadharisha kutoshangilia sana juu ya ujio wa kocha huyo.

Akizungumza na Spoti Xtra, mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe alisema kuwa makocha wengi waliopita klabuni hapo walikuwa ni wazuri lakini wachezaji siku zote ndiyo ambao wamekuwa wakiwaangusha kutokana na uwezo.

“Kwa hiyo, Wanasimba wasishangilie sana juu ya ujio wa kocha huyo kwani mambo yanaweza kuwaendea vibaya na mwisho wa siku wakaanza kumlaumu,” alisema Tambwe ambaye pia amewahi kuitumikia timu hiyo msimu wa 2013/14.

Lakini pia, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema; “Endapo atataka kuja na mfumo wake mwingine katika kipindi hiki ndoto zao za kuchukua ubingwa huo zinaweza kupotea kama misimu mingine iliyopita ambapo hali hiyo imekuwa ikiitesa timu hiyo.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here