MECHI ya Azam na Yanga itapigwa Jumamosi saa 1 usiku, ndani ya Azam Complex.

Mara ya mwisho Yanga kucheza mechi ya Ligi kwenye Uwanja huo ilikuwa msimu wa 2011 dhidi ya African Lyon ikiwa chini ya Kocha Sam Timbe.

Yanga haikuwahi kwenda Chamazi kucheza mechi ya Ligi nyakati za usiku tangu Uwanja huo uanzishwe na klabu hiyo tajiri nchini.

Uamuzi wa Azam kutumia Uwanja wake wa nyumbani kwenye mechi za Simba na Yanga badala ya ule wa Uhuru, umeanza kuwekewa mkazo na uongozi mpya wa TFF, chini ya Walace Karia.

Martha Mboma

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here