Droo ya 16 ya Kombe la FA imechezeshwa leo Alhamisi Jijini Dar es Salaam huku Yanga ikipangwa na Majimaji ya Songea na Azam na KMC.
Mechi hizo zitachezwa kati ya Februari 22 mpaka 25 kwenye Viwanja mbalimbali. Stand Utd imepangwa na Dodoma huku JKT Tanzania ikiikwaa Ndanda.
Kiluvya watacheza na Prisons, wakati Singida ikikipiga na Polisi Tanzania mjini Singida, huku Njombe ikicheza na Mbao.
Buseresere ambayo ndiyo timu ya daraja la chini iliyobaki kwenye michuano hiyo itacheza na Mtibwa mjini Geita.
Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho mwakani. Bingwa mtetezi ambaye ni Simba tayari ameshautema ubingwa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here