Hatua ya mzunguko wa Nne(4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inaendelea Jumamosi Februari 24, 2018 kwa michezo miwili.
Singida United watakuwa Uwanja wa Namfua Mjini Singida kucheza na Polisi Tanzania saa 10 jioni na mchezo mwingine utakaohitimisha siku hiyo utakuwa kati ya KMC watakaokuwa nyumbani Azam Complex, Chamazi kuwakaribisha Azam FC saa 1 usiku.
Mzunguko huo wa Nne(4) utaendelea tena Jumapili Februari 25, 2018 kwa Buseresere kuwaalika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nyamagana Mwanza mchezo utakaochezwa saa 8 mchana wakati Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam mchezo ukichezwa saa 10 jioni nao Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania Azam Complex Chamazi saa 1 usiku.
Mzunguko huwa wa 4 utakamilika Jumatatu Februari 26, 2018 Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
Ratiba Nzima ya Kombe la shirikiso Mzunguko wa 4
Tarehe Mechi Uwanja Muda
Februari 24, 2018 Singida United Vs Polisi Tanzania Namfua Mjini Singida saa 10 jioni
Februari 24, 2018 KMC Vs Azam FC Azam Complex saa 1 jioni
Februari 25, 2018 Buseresere Vs Mtibwa Sugar Nyamagana Mwanza saa 8 mchana
Februari 25, 2018 Majimaji FC Vs Young Africans Majimaji Songea saa 10 jioni
Februari 25, 2018 JKT Tanzania FC Vs Ndanda FC Azam Complex saa 1 jioni
Februari 26, 2018 Kiluvya United FC Vs Tanzania Prisons Mabatini saa 8 mchana
Februari 26, 2018 Stand United FC Vs Dodoma FC Kambarage saa 10 jioni

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here