MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
Dk 90, Yanga wanapeleka shambulizi ndani ya lango la Ndanda, lakini Ngassa anaokoa
Dk 88, kona inachongwa na Mwashiuya lakini mwamuzi anasema ni faulo
Dk 88, Mhilu anaingia vizuri kabisa hapa, mpira wake wa krosi unaondolewa na kuwa kona ya Yanga
DK 86 Martin anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Yusuf Mhilu upande wa Yanga
KADI Dk 85 Ahmed Msumi wa Ndanda analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Yondani
Dk 82 Ndanda FC wanafanya shambulizi kali hapa, inaokolewa, shuti jingine linagonga mtambaa wa panya na Yanga wanaokoa
KADI Dk 80, Mwashiuya analambwa kadi ya njano baada ya kuurusha mpira nje kwa jazba
Dk 78, Ngassa anawachambua Yanga na Yondani analazimika kumuweka chini hapa lakini anasalimika kadiSUB Dk 77 Ally Selemani anaingia upande wa Ndanda kuchukua nafasi ya TibaDk 76 John George anatandika mkwaju matata kabisa wa adhabu lakini kidogo unapita juu ya mtambaa wa panya wa lango la Yanga, goal kick
Dk 74, mkwaju safi wa adhabu karibu na lango la Ndanda lakini kuna wachezaji wa Yanga wameishaotea
Dk 73, Kessy anaingia vizuri kabisa upande wa mashariki lakini anawekwa chini na mwamuzi anasema faulo ipikwe kwenda Ndanda
Dk 72, kona inachongwa na Mwashiuya lakini Ndanda wanaondosha hapa
Dk 71, Ndanda wanalazimika kufanya kazi ya ziada, wanaokoa na kuwa konaaaa
Dk 70 mchezaji mmoja wa Ndanda yuko chini, inaonekana amelala mwenye inawezekana ni maumivu ya misuli
Dk 69 Yanga wanachofanya wanapeleka mashambulizi mengi ya juujuu
Dk 68 Makapu anaachia shuti kuuuuuuubwaaaa…goal kick
KADI Dk 65 Raphael Daud analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngassa
Dk 62 Majogoro anaingia vizuri akigongeana na Ngassa, anaachia mkwaju mkali hapa, goal kick
Dk 58 Ndanda wanaonekana wametawala sehemu ya kiungo na kupeleka mashambulizi mengi zaidi na Yanga wanapaswa kuwa makini
Dk 55, Ndanda wanasukuma shambulizi jingine lakini safari hii Rostand anakuwa makini ziaidi
DK 50 Raphael Daud yuko chini pale akimlalamikia mwamuzi namna alivyoangushwa. Anatolewa nje kwenda kutibiwa
GOOOOOOOOO Dk 46, Kapama anaukwamisha mpira wavuni akiunganisha pasi safi kabisa ya Ngassa
Dk 45 Mechi inaanza kwa kasi Ndanda wakionekana wanataka bao la mapema ili kuwapa Yanga presha
SUB Dk 45 upande wa Yanga anatoka Tshishimbi na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
MAPUMZIKO DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Abdallah naye anaachia mkwaju lakini hakulenga lango
Dk 44, Majogoro naye anaachia mkwaju hapa lakini hakulenga lango
Dk 42, krosi nzuri ndani ya lango la Ndanda, Kisubi anatokea na kudaka vizuri kabisa hapa
SUB Dk 40 Waziri Majogoro anaingia kuchukua nafasi ta Baraka upande wa Ndanda
Dk 40, anakwenda kupiga Tshishimbi, kipa anadaka na kuuficha kabisa
GOOOOOOOOOOOOO Dk 39 KADI 37 John George analambwa kadi ya njano PENAAAAAAAAAAAAAAT Dk 36, Yanga wanapata penalti baada ya beki wa Zabron kuunawa
Dk 34, Yanga wanachofanya ni kuupoza mpira wakisikilizia mabao yao mawili lakini wanashambulia kwa kushtukiza kila wanapopata nafasi
Dk 32, Martib anaingia vizuri lakini anaanguka na kipa anauwahi mpira
GOOOOOOOOO Dk 29 Kessy anachambua kama karanga kabla ya kuandika bao saaaafi la pili
DK 28, pasi ya Buswita, Martin anajaribu lakini ni shuti mtoto
Dk 25 Yanga wanalazimika kumuweka chini Ngassa, lakini mpira faulo naye anapiga nyanya kabisa na Rostand kama maji anadaka
Dk 23 nafasi nzuri nyingine kwa Yanga, kipa anaugusa, Ndanda wanaokoa
Dk 20, kona maridadi ndani ya lango la Ndanda, kipa Kisubi, anatoka na kuupiga ngumi
Dk 20, Ajibu anaachia mkwaju matata kabisa lakini kipa anaokoa kwa umaridadi kabisa. Kona
Dk 19, Ndanda wanapata kona, inachongwa lakini Yondani anaruka na kuokoa
Dk 19, inachongwa faulo vizuri na Ajibu, inaokolewa vizuri
Dk 18, Yanga inapata adhabu nje kidogo ya eneo la Ndanda
DK 15, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini mpira wa shuti la tik taka, unaishia mikononi mwa Rostande
Dk 13, inaonekana kuna makosa mengi sana katika difensi ya Ndanda na wanapaswa kuwa makini
Dk 10 shuti kali katika lango la Yanga, safari hii kipa yuko makini anaokoa, unamtoka anadaka tena
Dk 8, kona nyingi ya Ndanda, lakini Yanga wako makini wanaokoa hapa
Dk 7, Ndanda wanapata kona, inachongwa hapa, Rostand anaokoa na kuwa kona tena
GOOOOOOOO Dk 6, Buswita anafunga kwa ulaiiiini baada ya uzembe wa kipa na mabeki.
Dk 4, Ngassa tena anaingia vizuri, anapiga shuti la chinichini, goal kick
Dk 3, Ngassa anaachia mkwaju mkali, nusura afunge lakini hakuwa makini
Dk 1 Ndanda FC ndiyo wanaanza kushambulia kwa kasi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here