KIKOSI cha timu ya taifa, Taifa Stars, leo saa tisa alasiri kinatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Algeria kwa mchezo wa kirafiki ambao utapigwa siku ya Machi 22, mwaka huu.

Stars itaondoka na nyota wake kadhaa huku wengine wataungana na kikosi hicho wakitokea nchi tofauti ambako wanacheza soka.
Meneja wa Stars, Danny Msangi, alisema kuwa wachezaji wa nje wataungana na timu hiyo kutokea nchi wanazocheza.

“Wachezaji kama Samatta(Ubelgji), Msuva (Morocco), na Mandawa (Botswana) hawa watatokea nchi ambazo wapo huku lakini wale wa Simba wataungana na timu hiyo wakitokea Misri kwenye majukumu ya klabu yao,” alisema Msangi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here